ETE Mtandaoni vs ETE ya Jadi
Linganisha mifumo miwili ya kujifunza na uchague inayokufaa wewe na kikundi chako.
Njia Mbili, Lengo Moja: Kukua katika Kristo
Programu ya Elimu ya Theolojia kwa Enezi (ETE) ya Ukanda wa Kusini imekuwa baraka kubwa kwa wengi katika kuwajenga watumishi imara katika Neno la Mungu.
Ili kuwafikia watu wengi zaidi katika mazingira tofauti, sasa tunatoa programu yetu pendwa ya ETE katika mifumo mikuu miwili: ETE ya Jadi (kwa kutumia vitabu) na ETE Mtandaoni (kwa kutumia simu janja).
Jambo la muhimu: Ingawa njia za kujifunzia zinatofautiana, moyo, lengo, na teolojia ya programu ya ETE ni ile ile. Zote zinalenga kukujenga wewe na kikundi chako katika Kristo.
ETE ya Jadi (Mfumo wa Vitabu)
Huu ndio mfumo tuliozoea na kuutumia kwa miaka mingi. Ni mfumo imara unaotegemea nguvu ya neno lililoandikwa.
Wanafunzi hupewa vitabu vilivyochapishwa vyenye masomo yote. Mwanafunzi anasoma somo husika nyumbani kwake kabla ya kukutana na kikundi.
Inafaa kwa:
- Maeneo ambayo hayana umeme wa uhakika au mtandao wa intaneti
- Watu wanaopendelea kusoma na kushika kitabu halisi mkononi
- Wale wasiomudu au wasio na simu janja (smartphone)
Mahitaji
- • Kitabu cha ETE
- • Kalamu na daftari
- • Uwezo wa kusoma
Mahitaji
- • Simu janja (smartphone)
- • Upatikanaji wa intaneti
- • Programu ya ETE au tovuti
- • Uwezo wa kusoma
ETE Mtandaoni (Mfumo wa Kidijitali)
Huu ni mfumo mpya unaotumia teknolojia ya kisasa kuleta mafundisho karibu nawe kupitia simu yako.
Katika ETE mtandaoni unasoma somo lile lile lililo katika kitabu, lakini unalipata kwenye simu: pamoja na picha, pamoja na somo lililosomwa kwa sauti ili uweze kusikiliza unaposoma, na pamoja na maswali unayojibu papo hapo na kupata jibu mara moja.
Kwa hiyo unahitaji uwezo wa kusoma pia katika ETE mtandaoni. Ni maandishi yale yale ya kitabu, na maswali unayasoma mwenyewe. Sauti ni msaada — haibadilishi kusoma.
Inafaa kwa:
- Watu wenye simu janja na wanaoweza kupata intaneti
- Watu wanaotaka kusikiliza somo wakati wanalisoma
- Watu wanaopenda kutumia teknolojia katika kujifunza
MUHIMU: Njia ya Ujifunzaji Haijabadilika
Hili ndilo jambo la msingi zaidi! Iwe unasoma katika kitabu au kwenye simu, moyo wa ETE upo kwenye kikundi.
Mikutano ni LAZIMA
Washiriki ni lazima wakutane kwenye vikundi vidogo: vikundi vingi kila baada ya wiki mbili, vingine kila wiki.
Majadiliano ni Kiini
Lengo la kukutana ni kujadili kwa pamoja maswali yaliyoibuliwa na somo mlilojifunza.
Ushirika na Ukuaji
Tunajifunza kutoka kwa kila mmoja, tunaombeana, na tunakua pamoja katika imani.
Jedwali la Mlinganisho
| Kipengele | ETE ya Jadi | ETE Mtandaoni |
|---|---|---|
| Nyenzo Kuu | Vitabu vilivyochapishwa | Somo lile lile la kitabu, kwenye simu |
| Mahitaji ya Msingi | Kitabu na uwezo wa kusoma | Simu janja, intaneti na uwezo wa kusoma |
| Mtindo wa Kujifunza | Kwa kusoma | Kwa kusoma, na sauti kama msaada |
| Eneo Linalofaa | Popote, hasa pasipo mtandao | Popote penye intaneti |
| Mikutano ya Kikundi | LAZIMA | LAZIMA |
Uko Tayari Kuanza Safari Yako?
Zungumza na wenzako katika kikundi chenu au mchungaji wako ili mchague mfumo unaowafaa zaidi.
Jiandikishe